أَوَلَمۡ يَهۡدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ أَهۡلِهَآ أَن لَّوۡ نَشَآءُ أَصَبۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡۚ وَنَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ
Je, hawahidiki hawa wanao rithi ardhi baada ya wale wenyewe kwamba tukitaka tutawapatiliza kwa madhambi yao, na tutapiga muhuri juu ya nyoyo zao, na kwa hivyo hawatasikia?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kwani haikuwafunukia wale waliokaa kwenye nchi baada ya watu wake waliopita kuangamizwa kwa maasia yao, na wakafuata miendo yao, kwamba lau tunataka tungaliwaadhibu kwa makosa yao, kama tulivyowafanyia waliopita kabla yao, na kwamba tutazipiga chapa nyoyo zao, haki isiingie na wasisikie mawaidha wala makumbusho?
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس