ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَظَلَمُواْ بِهَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Kisha baada yao tukamtuma Musa na Ishara zetu kwa Firauni na waheshimiwa wake. Nao wakazikataa. Basi tazama ulikuwaje mwisho wa waharibifu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kisha tulimtuma, baada ya Mitume waliotangulia kutajwa, Mūsā mwana wa 'Imrān kwa miujiza yetu iliyo wazi aende kwa Fir'awn na watu wake, wakaikataa na kuikanusha kwa udhalimu na upinzani. Tazama kwa mazingatio, namna gani tuliwafanya na tuliwazamisha hadi wa mwisho wao, huku Mūsā na watu wake wakiona? Na huo ndio mwisho wa waharibifu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس