قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱللَّهِ وَٱصۡبِرُوٓاْۖ إِنَّ ٱلۡأَرۡضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ
Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho ni wa wachamngu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Akasema Mūsā kuwaambia watu wake, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, «Takeni msaada kwa Mwenyezi Mungu Awaokoe na Fir'awn na watu wake, na subirini juu ya shida zinazowapata nyinyi na watoto wenu kutoka kwa Fir 'awn. Kwani ardhi yote ni ya Mwenyezi Mungu Anamrithisha Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na mwisho mwema ni wa anyemcha Mwenyezi Mungu akafanya maamrisho Yake na akajiepusha na makatazo Yake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس