قَالَ رَبِّ ٱغۡفِرۡ لِي وَلِأَخِي وَأَدۡخِلۡنَا فِي رَحۡمَتِكَۖ وَأَنتَ أَرۡحَمُ ٱلرَّـٰحِمِينَ
(Musa) akasema: Mola Mlezi wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu, na ututie katika rehema yako. Nawe ni Mwenye kurehemu kushinda wote wenye kurehemu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mūsā Alisema, ulipomfunukia udhuru wa ndugu yake na kujua kuwa yeye hakufanya uzembe katika kusimama imara juu ya amri ya Mwenyezi Mungu, «Mola wangu nisamehe ghadhabu zangu na umsamehe ndugu yangu yaliyopita kati yake na Wana wa Isrāīl, na ututie ndani ya rehema yako kunjufu, kwani wewe una huruma na sisi zaidi kuliko kila mwenye huruma.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس