وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى ٱلۡغَضَبُ أَخَذَ ٱلۡأَلۡوَاحَۖ وَفِي نُسۡخَتِهَا هُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلَّذِينَ هُمۡ لِرَبِّهِمۡ يَرۡهَبُونَ
Na Musa ilipo mtulia ghadhabu aliziokota zile mbao. Na katika maandiko yake mna uwongofu na rehema kwa wanao mwogopa Mola wao Mlezi.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Zilipotulia hasira za Mūsā alizichukua mbao baada ya kuwa alizitupa chini, na ndani yake mlikuwa na maelezo ya haki na rehema kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu na kuogopa mateso Yake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس