قَالَ ٱخۡرُجۡ مِنۡهَا مَذۡءُومٗا مَّدۡحُورٗاۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akasema, kumwambia Iblisi, «Toka Peponi ukiwa umechukiwa na umefukuzwa. Nitaujaza Moto wa Jahanamu kwa kukuingiza wewe humo na binadamu wote watakaokufuata.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس