إِنَّ ٱلَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَيُسَبِّحُونَهُۥ وَلَهُۥ يَسۡجُدُونَۤ۩
Hakika wale walioko kwa Mola wako Mlezi hawajivuni wakaacha kumuabdu, na wanamtakasa na wanamsujudia.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika wale waliyoko mbele ya Mola Wako miongoni mwa Malaika hawafanyi kiburi kwa kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, bali wao wanaandama amri Zake, wanamtakasa mchana na usiku na wanamwepusha na mambo yasiyonasibiana na Yeye, na Yeye Peke Yake wanamsujudia.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس