فَدَلَّىٰهُمَا بِغُرُورٖۚ فَلَمَّا ذَاقَا ٱلشَّجَرَةَ بَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۖ وَنَادَىٰهُمَا رَبُّهُمَآ أَلَمۡ أَنۡهَكُمَا عَن تِلۡكُمَا ٱلشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَآ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمَا عَدُوّٞ مُّبِينٞ
Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa dhaahiri?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hapo yeye aliwatia wao ujasiri na akawadanganya wakala kutoka mti huo ambao Mwenyezi Mungu Aliwakataza wasiukaribie. Walipokula kutoka mti huo, ziliwafunuka tupu zao na kikaondoka kile ambacho Mwenyezi Mungu Aliwasitiri nacho kabla ya wao kufanya uhalifu huo, wakawa wanayaambatisha majani ya miti ya Peponi kwenye tupu zao. Hapo Mola wao, Aliyetukuka na kuwa juu, Aliwaita, «Kwani sikuwakataza kula kutoka mti ule na nikawaambia kwamba Shetani, kwenu nyinyi, ni adui ambaye uadui wake uko waziwazi?» Katika aya hii kuna ushahidi kwamba kukaa uchi ni kati ya mambo makubwa na kwamba hilo ni jambo lililokowa lachukiza na linaloendelea kuchukiza katika tabia, na ni ovu kwenye akili za watu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس