ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ دِينَهُمۡ لَهۡوٗا وَلَعِبٗا وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَاۚ فَٱلۡيَوۡمَ نَنسَىٰهُمۡ كَمَا نَسُواْ لِقَآءَ يَوۡمِهِمۡ هَٰذَا وَمَا كَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَجۡحَدُونَ
Ambao waliifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo Sisi tunawasahau kama walivyo usahau mkutano wa Siku yao hii, na kwa sababu ya kule kuzikataa Ishara zetu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wale ambao Mwenyezi mungu, Aliyetukuka, Atawanyima starehe za Akhera ni wale ambao waliifanya Dini, ambayo Mwenyezi Mungu Amewaamuru kuifuata, kuwa ni pumbao, na yakawadanganya wao maisha ya ulimwenguni, wakashughulishwa na mapambo yake wasifanye matendo ya kuwafaa Akhera, hao Atawasahau Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama, na Atawaacha ndani ya adhabu iumizayo, kama walivyoyaacha matendo ya kuwafaa kwa kukutana na Siku yao hii, na kwa kuwa wao walikuwa wakizikanusha dalili za Mwenyezi Mungu na hoja Zake pamoja na kujua kwao kuwa ni za ukweli.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس