وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَتَأۡتُونَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na tulimtuma Lut', alipo waambia watu wake: Je, mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote kwa uchafu huo katika viumbe vyote!
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na mkumbuke, ewe Mtume, Lūṭ, amani imshukie, pindi aliposema kuwaambia watu wake, «Je, mnafanya kitendo kibaya kilichofikia upeo wa ubaya? Hakuna yoyote, miongoni mwa viumbe, aliyefanya kitendo hiko kabla yenu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس