وَمَا وَجَدۡنَا لِأَكۡثَرِهِم مِّنۡ عَهۡدٖۖ وَإِن وَجَدۡنَآ أَكۡثَرَهُمۡ لَفَٰسِقِينَ
Wala hatukuwaona wengi wao kuwa wanatimiza ahadi; bali kwa hakika tuliwakuta wengi wao ni wapotofu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na hatukuwapata wengi wa watu waliopita kuwa wana uaminifu wala utekelezaji ahadi, na hatukuwapata wengi wao isipokuwa ni watokaji nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na ufuataji amri Yake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس