فَإِذَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡحَسَنَةُ قَالُواْ لَنَا هَٰذِهِۦۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةٞ يَطَّيَّرُواْ بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓۗ أَلَآ إِنَّمَا طَـٰٓئِرُهُمۡ عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Likiwafika jema wakisema: Haya ni haki yetu. Na likiwafika ovu husema: Musa na walio pamoja naye ni wakorofi. Hakika ukorofi wao huo unao wafikia unatoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Ukiwajia Fir'awn na watu wake urutuba na chakula huwa wakisema, «Hii ni yetu tunayoistahiki.» Na ukiwapata wao ukame na chaka huwa wakiona wameingiliwa na ukorofi na huwa wakisema, «Haya ni kwa sababu ya Mūsā na walio pamoja na yeye.»Jua utanabahi kwamba yanayowapata ya ukame na chaka ni kwa uamuzi wa Mwenyezi Mungu na makadirio Yake, na ni kwa sababu ya madhambi yao na ukafiri wao. Lakini wengi wa watu wa Fir'awn hawalijui hilo, kwa kuvama kwao kwenye ujinga na upotevu.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس