وَٱتَّخَذَ قَوۡمُ مُوسَىٰ مِنۢ بَعۡدِهِۦ مِنۡ حُلِيِّهِمۡ عِجۡلٗا جَسَدٗا لَّهُۥ خُوَارٌۚ أَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّهُۥ لَا يُكَلِّمُهُمۡ وَلَا يَهۡدِيهِمۡ سَبِيلًاۘ ٱتَّخَذُوهُ وَكَانُواْ ظَٰلِمِينَ
Na baada yake walimfanya ndama kutokana na mapambo yao (kumuabudu), kiwiliwili tu kilicho kuwa na sauti. Hivyo, hawakuona kuwa hawasemezi wala hawaongoi njia? Wakamuabudu, na wakawa wenye kudhulumu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na walitengeneza watu wa Mūsā, baada ya yeye kuwaacha kwenda kuzungumza na Mola Wake, sanamu wa kigombe asiye na roho anayetoa sauti, kutokana na dhahabu yao, wakamfanya ni muabudiwa. Kwani hawajui kwamba yeye hasemi na wao na hawaongozi wao kwenye kheri yoyote? Walijasiri kufanya jambo hili ovu, wakawa ni wenye kujidhulumu nafsi zao, ni wenye kuweka kitu mahala pasipokuwa pake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس