فَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ قَوۡلًا غَيۡرَ ٱلَّذِي قِيلَ لَهُمۡ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِجۡزٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُواْ يَظۡلِمُونَ
Lakini walio dhulumu miongoni mwao walibadilisha kauli, sio ile waliyo ambiwa. Basi tukawapelekea adhabu kutoka mbinguni kwa vile walivyo kuwa wakidhulumu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Waliomkanusha Mwenyezi Mungu kati yao waliligeuza neno ambalo Mwenyezi Mungu Aliwaamrisha waliseme, wakaingia mlangoni wakijikokota kwa matako yao na wakasema, «habbah fī sha'rah» (mbegu kwenye unywele), hapo tukawateremshia adhabu kutoka mbinguni, tukawaangamiza kwayo, kwa sababu ya udhalimu wao na uasi wao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس