وَإِذۡ قَالَتۡ أُمَّةٞ مِّنۡهُمۡ لِمَ تَعِظُونَ قَوۡمًا ٱللَّهُ مُهۡلِكُهُمۡ أَوۡ مُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗاۖ قَالُواْ مَعۡذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ
Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamchamngu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi kundi kati yao waliposema kuwaambia kundi lingine lililokuwa likiwapa mawaidhia wale waliopita mipaka siku ya Jumamosi na likiwakataza wasimuasi Mwenyezi Mungu siku hiyo, «Kwa nini nyinyi mnawaidhia watu ambao Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangamiza ulimwenguni kwa kumuasi au ni Mwenye kuwaadhibu adhabu kali kesho Akhera?» Wakanena wale waliokuwa wakiwakataza wasimuasi Mwenyezi Mungu, «Tunawaidhia na tunawakataza ili tuwe na udhuru kuhusu wao na kwa ajili ya kutekeleza wajibu wa Mwenyezi Mungu juu yetu ya kuamrisha mema na kukataza maovu na kwa matumaini kwamba watamcha Mwenyezi Mungu, watamuogopa na watatubia kutokana na kumuasi kwao Mola wao na kupita mipaka ya mambo yaliyoharamishiwa kwao.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس