وَقَطَّعۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ أُمَمٗاۖ مِّنۡهُمُ ٱلصَّـٰلِحُونَ وَمِنۡهُمۡ دُونَ ذَٰلِكَۖ وَبَلَوۡنَٰهُم بِٱلۡحَسَنَٰتِ وَٱلسَّيِّـَٔاتِ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ
Na tuliwafarikisha katika ardhi makundi makundi. Wako kati yao walio wema, na wengine kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mema na mabaya ili wapate kurejea.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na tuliwagawanya Wana wa Isrāīl makundi: kati yao kuna wanaosimama kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja Wake, na kati yao kuna wenye kufanya kasoro wenye kuzidhulumu nafsi zao. Na hawa tuliwapa mtihani wa maisha ya neema na ukunjufu wa riziki; na pia tuliwapa mtihani wa maisha ya dhiki, misiba na matatizo kwa matarajio kuwa watarudi kumtii Mola wao na watatubia kutokana na vitendo vya kumuasi.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس