وَإِذۡ أَخَذَ رَبُّكَ مِنۢ بَنِيٓ ءَادَمَ مِن ظُهُورِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَأَشۡهَدَهُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَلَسۡتُ بِرَبِّكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ شَهِدۡنَآۚ أَن تَقُولُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّا كُنَّا عَنۡ هَٰذَا غَٰفِلِينَ
Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Mola wako Alipowatoa wana wa Ādam kutoka kwenye migongo ya baba zao, Akawathibitishia upweke Wake kwa kuwatia tabia ya kimaumbile kwamba Yeye ni Mola wao, ni Muumba wao na ni Mmiliki wao; wakamkubalia hilo kwa kuchelea wasije kukanusha Siku ya Kiyama wasikubali chochote katika hilo na wasije wakadai kwamba hoja ya Mwenyezi Mungu haijasimama kwao na wala hawajui chochote juu yake, bali wao walikuwa wameghafilika na hilo.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس