وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱلَّذِيٓ ءَاتَيۡنَٰهُ ءَايَٰتِنَا فَٱنسَلَخَ مِنۡهَا فَأَتۡبَعَهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَكَانَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ
Na wasomee khabari za yule ambaye tulimpa Ishara zetu, naye akajivua nazo. Na Shet'ani akamuandama, akawa miongoni walio potea.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na wasimulie,ewe Mtume, watu wako habari ya mwanamume mmoja miongoni mwa Wana wa Isrāīl, tuliyompa hoja zetu na dalili zetu, akajifunza hizo kisha akazikanusha na akazitupa nyuma ya mgongo wake, akashindwa na Shetani na akawa ni miongoni mwa wapotevu wenye kuangamia, kwa sababu ya kuenda kinyume kwake na amri ya Mola wake na kumtii kwake Shetani.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس