إِنَّ وَلِـِّۧيَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى ٱلصَّـٰلِحِينَ
Hakika Mlinzi wangu ni Mwenyezi Mungu aliye teremsha Kitabu. Naye ndiye awalindae walio wema.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
«Hakika mtegemewa wangu ni Mwenyezi Mungu Ambaye Anasimamia kunihifadhi na kunipa ushindi. Yeye Ndiye Ambaye Aliniteremshia Qur’ani kwa haki na Yeye Anawasimamia walio wema miongoni mwa waja wake na anawapa ushindi juu ya maadui zao na Haachi kuwasaidia.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس