أَوَعَجِبۡتُمۡ أَن جَآءَكُمۡ ذِكۡرٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ مِّنكُمۡ لِيُنذِرَكُمۡ وَلِتَتَّقُواْ وَلَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Je, mnastaajabu kukujieni mawaidha yanayotoka kwa Mola Mlezi wenu kwa njia ya mtu aliye ni mmoja katika nyinyi, ili akuonyeni na ili mumchemngu, na ili mpate kurehemewa?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
«Je imewafanya nyinyi muone ajabu kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameteremsha kwenu yale ambayo yatawakumbusha mambo yenye kheri kwenu, kwa ulimi wa mtu miongoni mwenu, mnaoujua ukoo wake na ukweli wake, ili awaogopeshe adhabu ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na mateso Yake, na ili mujikinge na hasira Zake kwa kumuamini na kwa kutarajia kufaulu kupata rehema Zake na malipo Yake mema mengi?
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس