فَعَقَرُواْ ٱلنَّاقَةَ وَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ وَقَالُواْ يَٰصَٰلِحُ ٱئۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na wakamuuwa yule ngamia, na wakaasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe Saleh! Tuletee unayo tuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wakamchinja ngamia kwa kutojali onyo la Ṣāliḥ, na wakaingiwa na kiburi kilichowafanya wasifuate amri ya Mola wao na wakasema, kwa njia ya shere na kwa kuona kuwa adhabu iko mbali na wao, «Ewe Ṣāliḥ, tuletee hiyo adhabu ambayo unatuonya nayo, iwapo wewe ni miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu!»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس