إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٌ أُوْلَـٰٓئِكَ عَلَيۡهِمۡ لَعۡنَةُ ٱللَّهِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ
Hakika walio kufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika wale waliokanusha imani na wakaficha haki na wakaendelea hivyo mpaka kufa kwao, juu yao kuna laana ya Mwenyezi Mungu na Malaika na watu wote kwa kuwatoa kwenye rehema Yake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس