حَقِيقٌ عَلَىٰٓ أَن لَّآ أَقُولَ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ قَدۡ جِئۡتُكُم بِبَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَرۡسِلۡ مَعِيَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ
Inafaa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila lilio la Haki. Nami hakika nimekujieni na dalili waziwazi kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi waache Wana wa Israili wende nami.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
«Nastahili nisiseme kuhusu Mwenyezi Mungu isipokuwa ukweli na inapasa kwangu nijilazimishe nayo. Nimewajia na dalili na hoja zenye ushindi kutoka kwa Mola wenu juu ya ukweli wa yale ninayowatajia. Basi waachilie, ewe Fir'awn, Wana wa Isrāīl pamoja na mimi kutoka kwenye kifungo chako na ukandamizaji wako, na wape uhuru wa kumuabudu Mwenyezi Mungu.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس