وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّـٰظِرِينَ
Na akatoa mkono wake, mara ukawa mweupe kwa watazamao.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na akauvuta mkono wake kutoka kwenye uwazi wa kanzu iliyofunguliwa kifuani au chini ya kapwa lake, na papo hapo ukawa mweupe kama maziwa usio na mbalanga, ukiwa ni alama kwa Fir'awn; akiurejesha unarudi rangi yake ya mwanzo, kama ulivyo mwili wake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس