فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ فَأَغۡرَقۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ بِأَنَّهُمۡ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُواْ عَنۡهَا غَٰفِلِينَ
Basi tuliwapatiliza, tuka- wazamisha baharini kwa sababu walizikanusha Ishara zetu, na wakaghafilika nazo.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Basi tukawalipiza ulipokuja muda uliowekwa kwa wao kuangamizwa, kwa kuwashushia mateso yetu, nayo ni kuwazamisha baharini, kwa sababu ya kuikanusha kwao miujiza iliyodhihiri kwa Mūsā na wakawa wanaipuuza; na kupuuza huko ndio sababu ya kukanusha.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس