وَأَوۡرَثۡنَا ٱلۡقَوۡمَ ٱلَّذِينَ كَانُواْ يُسۡتَضۡعَفُونَ مَشَٰرِقَ ٱلۡأَرۡضِ وَمَغَٰرِبَهَا ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَاۖ وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ ٱلۡحُسۡنَىٰ عَلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ بِمَا صَبَرُواْۖ وَدَمَّرۡنَا مَا كَانَ يَصۡنَعُ فِرۡعَوۡنُ وَقَوۡمُهُۥ وَمَا كَانُواْ يَعۡرِشُونَ
Na tukawarithisha watu walio kuwa wanadharauliwa mashariki na magharibi ya ardhi tuliyo ibariki. Na likatimia neno jema la Mola Mlezi wako juu ya Wana wa Israili, kwa vile walivyo subiri. Na tukayaangamiza aliyo kuwa akiyafanya Firauni na kaumu yake, na waliyo kuwa wakiyajenga.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Tukawarithisha Wana wa Isrāīl, waliokuwa wakifanywa wanyonge, pande za mashariki na magharibi ya ardhi, nazo ni sehemu za miji ya Sham, tulizozitia baraka kwa kutoa mazao na matunda na mito. Na limetimia neno jema la Mola wako, ewe Muhammad, kwa Wana wa Isrāīl kwa kuwapa utulivu katika ardhi kwa sababu ya kuvumilia kwao makero ya Fir'awn na watu wake. Na tukayavunjavunja yale maamirisho na mashamba ambayo Fir'awn na watu wake walikuwa wakiyatengeneza, na majengo na majumba na mengineyo waliokuwa wakiyajenga.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس