وَٱلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِهَا وَءَامَنُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na walio tenda maovu, kisha wakatubia baada yake na wakaamini, hapana shaka kuwa Mola Mlezi wako baada ya hayo ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na wale waliofanya maovu ya ukafiri na maasia kisha wakarejea, baada ya kuyafanya, kwenye Imani na matendo mema, hakika Mola wako baada ya toba ya kidhati ni Msamehefu mno wa vitendo vyao viovu si Mwenye kuwafedhehi kwavyo, ni Mwenye kuwarehemu wao na kila aliye mfano wao miongoni mwa wenye kutubia.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس