وَٱلَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِٱلۡكِتَٰبِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُصۡلِحِينَ
Na wale wanao kishikilia Kitabu, na wakashika Sala - hakika Sisi hatupotezi ujira wa watendao mema.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na wanaoshikamana na Kitabu, wanaoyafuata kivitendo yaliyomo ndani yake miongoni mwa mambo ya itikadi na hukumu na wanaodumu na Swala kwa mipaka yake na wasiyozipoteza nyakati zake, Mwenyezi Mungu Atawalipa kwa matendo yao mema na hatayapoteza.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس