أَوۡ تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أَشۡرَكَ ءَابَآؤُنَا مِن قَبۡلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةٗ مِّنۢ بَعۡدِهِمۡۖ أَفَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ
Au mkasema: Hakika baba zetu ndio walio shirikisha kabla yetu, na sisi ni dhuriya zao tu baada yao. Basi utatuangamiza kwa sababu ya waliyo yafanya wapotovu?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na ili msiseme, «Hakika baba zetu walishirikisha kabla yetu na wakavunja ahadi, na sisi tukawafuata, basi je utatuadhibu kwa yale waliyoyafanya wale ambao waliyaharibu matendo yao kwa kumfanya Mwenyezi Mungu ana mshirika katika ibada?»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس