أَوَلَمۡ يَتَفَكَّرُواْۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Je, hawafikiri? Huyu mwenzao hana wazimu. Hakuwa yeye ila ni mwonyaji aliye dhaahiri.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kwani hawafikirii hawa ambao walizikanusha aya zetu wakazingatia kwa akili zao na wakajua kwamba Muhammad hana wazimu? Yeye hakuwa isipokuwa ni mwenye kuwaonya wao mateso ya Mwenyezi Mungu kwa kumkanusha kwao Yeye, iwapo hawataamini, na ni mshauri muaminifu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس