۞يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ خُذُواْ زِينَتَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya israfu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Enyi wanadamu! Kuweni, kila mnapotekeleza Swala, katika hali ya pambo linalokubalika kisheria la nguo zinazofinika tupu zenu na muwe katika hali ya usafi, utohara na mfano wake. Na kuleni na kunyweni katika vizuri Alivyowapa Mwenyezi Mungu, wala msikiuke mipaka ya wastani, kwani Mwenyezi Mungu Hawapendi wakiukaji wenye kupitsha kiasi katika vyakula na vinywaji na mengineyo.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس