قُلۡ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَ وَٱلۡإِثۡمَ وَٱلۡبَغۡيَ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَأَن تُشۡرِكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗا وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asicho kiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema,ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyeyafanya matendo maovu kuwa ni haramu, yale yaliyo waziwazi na yale yaliyofichika, na Ameyakataza maasia yote, na miongoni mwa makubwa zaidi ya maasia ni kuwafanyia watu uadui, kwani hilo liko kando na haki. Na Amewaharamishia kuabudu, pamoja na Mwenyezi Mungu, Aliyetuka, vitu vyingine kati ya vile ambavyo Hakuviteremshia ushahidi wala hoja, kwani afanyaye hayo hana kithibitisho chochote. Na Amewaharamishia kumnasibishia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, sheria ambayo Hakuipasisha kwa kumzulia urongo,» kama madai ya kwamba Mwenyezi Mungu Ana mwana na kuharamisha baadhi ya vilivyo halali katika mavazi na chakula.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس