وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٞۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ لَا يَسۡتَأۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ
Na kila umma una muda wake. Utakapo fika muda wao basi hawatakawia hata saa moja, wala hawatatangulia.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kila kikundi kilichojikusanya kumkanusha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na kuwakanusha Mitume Wake, amani iwashukie, kina wakati wa kushukiwa na mateso. Huo wakati, Aliouweka Mwenyezi Mungu wa kuwaangamiza, hawatakawia nao, japokuwa kwa muda mfupi, wala hawataungulia.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس