وَهُوَ ٱلَّذِي يُرۡسِلُ ٱلرِّيَٰحَ بُشۡرَۢا بَيۡنَ يَدَيۡ رَحۡمَتِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَقَلَّتۡ سَحَابٗا ثِقَالٗا سُقۡنَٰهُ لِبَلَدٖ مَّيِّتٖ فَأَنزَلۡنَا بِهِ ٱلۡمَآءَ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِۚ كَذَٰلِكَ نُخۡرِجُ ٱلۡمَوۡتَىٰ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
Na Yeye ndiye anaye peleka pepo (za kuvuma) kuwa ni bishara kabla ya kufika rehema yake. Hata hizo pepo zinapo beba mawingu mazito tunayachunga mpaka kwenye nchi iliyo kufa. Kisha tunateremsha kwayo maji, ndio kama hivyo tukatolesha kila aina ya matunda. Basi hali kadhaalika tunavyo wafufua wafu, ili mpate kukumbuka.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Anayetuma upepo mzuri mororo wenye kubashiria mvua ambayo upepo huo unaisukuma kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na hapo viumbe vikangiwa na furaha kwa hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu. Na pindi ifikapo wakati ambapo upepo umebeba mawingu yaliyobebeshwa mvua, Mwenyezi Mungu Huyapeleka kwa upepo huo ili kuihuisha nchi iliyopigwa na ukame ardhi yake na kukauka miti yake na mimea yake ya nafaka, Mwenyezi Mungu hapo Akaiteremsha, kwa mawingu hayo, mvua, Akaitoa kwayo nyasi, miti na mimea ya nafaka, na miti ikarudi kujaa sampuli ya matunda. Kama tunavyoihuisha ardhi hii kwa mvua, vilevile tutawatoa wafu kutoka makabarini mwao baada ya kutoweka kwao, ili muwaidhike na mchukulie dalili juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu na uwezo Wake wa kufufua.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس