وَمَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُم بِمَا كَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَظۡلِمُونَ
Na watakao kuwa na uzani khafifu, basi hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzipinga Ishara zetu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na yoyote yule ambaye mizani za vitendo vyake zitakuwa nyepesi, kwa wingi wa maovu yake, hao ndio waliopoteza bahati yao ya kupata radhi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa sababu ya kukiuka kwao mipaka kwa kuzikanusha aya za Mwenyezi Mungu , Aliyetukuka, na kukosa kuzifuata.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس