ترجمة معاني سورة القارعة باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
ﰡ
آية رقم 1
ﭴ
ﭵ
Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu kwa vituko vyake.
آية رقم 2
ﭶﭷ
ﭸ
Ni kitu gani hiko chenye kugonga?
آية رقم 3
ﭹﭺﭻﭼ
ﭽ
Na ni lipi lililokujulisha ni kipi hiko chenye kugonga?
آية رقم 4
ﭾﭿﮀﮁﮂ
ﮃ
Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama pandzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni.
آية رقم 5
ﮄﮅﮆﮇ
ﮈ
Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa ni mapepe na ikamalizika.
آية رقم 6
ﮉﮊﮋﮌ
ﮍ
Basi mwenye kuwa mizani za mema yake ni nzito,
آية رقم 7
ﮎﮏﮐﮑ
ﮒ
atakuwa kwenye maisha ya kuridhika Peponi.
آية رقم 8
ﮓﮔﮕﮖ
ﮗ
Ama mwenye kuwa mizani za mema yake ni nyepesi na mizani za maovu yake ni nzito,
آية رقم 9
ﮘﮙ
ﮚ
makazi yake yatakuwa ni Moto wa Jahanamu.
آية رقم 10
ﮛﮜﮝﮞ
ﮟ
Ni lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni ipi hii Jahanamu inayoitwa «Hāwiyah»?
آية رقم 11
ﮠﮡ
ﮢ
Ni Moto unaowaka sana kwa kuni ziliomo ndani yake.
تقدم القراءة