ترجمة معاني سورة الفجر باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
ﰡ
آية رقم 1
ﭤ
ﭥ
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa alfajiri
آية رقم 2
ﭦﭧ
ﭨ
na masiku kumi ya kwanza ya Mfungotatu na kwa kile kilichoyafanya yawe matukufu,
آية رقم 3
ﭩﭪ
ﭫ
kwa kila idadi igawanyikayo na isiyogawanyika,
آية رقم 4
ﭬﭭﭮ
ﭯ
kwa usiku upitapo na giza lake.
آية رقم 5
ﭰﭱﭲﭳﭴﭵ
ﭶ
Kwani hakuna katika kiapo kiliyotajwa chenye kukinaisha kwa mwenye akili?
آية رقم 6
ﭷﭸﭹﭺﭻﭼ
ﭽ
Huoni, ewe Mtume, vipi Mola wako
آية رقم 7
ﭾﭿﮀ
ﮁ
Alivyoiangamiza kaumu ya Ād'. kabila la Irama lenye nguvu na majengo yaliyoinuliwa juu ya vipia,
آية رقم 8
ﮂﮃﮄﮅﮆﮇ
ﮈ
ambalo hakukuumbwa mfano wake katika miji, kwa ukubwa wa miili na wingi wa nguvu?
آية رقم 9
ﮉﮊﮋﮌﮍ
ﮎ
Na vipi Alivyowafanya Thamūd, kaumu ya Ṣāliḥ, ambao waliweza kuchonga jabali na kufanya nyumba ndani yake?
آية رقم 10
ﮏﮐﮑ
ﮒ
Na vipi Alivyomfanya Firauni, mfalme wa Misri, aliyekuwa na askari waliouhami ufalme wake na kuutilia nguvu.
آية رقم 11
ﮓﮔﮕﮖ
ﮗ
Hawa ndio waliokitumia nguvu na kudhulumu mijini.
آية رقم 12
ﮘﮙﮚ
ﮛ
Wakaeneza humo, kwa dhuluma zao, uharibifu.
آية رقم 13
ﮜﮝﮞﮟﮠ
ﮡ
Mwenyezi Mungu Akawamiminia adhabu kali.
آية رقم 14
ﮢﮣﮤ
ﮥ
Hakika Mola wako,ewe Mtume, Anamwangalia mwenye kumuasi kwa kumpa muhula kidogo, kisha Humpatiliza kwa uwezo na ushindi..
آية رقم 15
Huyu binadamu, Mola wake Anapompa mtihani wa neema, Anapomkunjulia riziki yake na kumpa maisha mazuri, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye ana cheo kwa Mola wake na huwa akisema :»Mola wangu Amenitukuza.»
آية رقم 16
Na Anapomuonja na Akambania riziki yake, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye amefanywa mnyonge na Mwenyezi Mungu na huwa akisema: «Mola wangu Amenifanya mnyonge.».
آية رقم 17
ﯞﯟﯠﯡﯢﯣ
ﯤ
Hali ya mambo si kama anavyodhania binadamu huyu, kwani mtu hutukuzwa kwa kumtii Mwenyzi Mungu na hufanywa mnyonge kwa kumuasi Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamwakirimu mayatima na kuwatendea wema.
آية رقم 18
ﯥﯦﯧﯨﯩ
ﯪ
Wala hamhimizani kulisha maskini.
آية رقم 19
ﯫﯬﯭﯮ
ﯯ
Na mnakula haki za watu, katika kurithi, kwa pupa.
آية رقم 20
ﯰﯱﯲﯳ
ﯴ
Na mnapenda mali kupita kiasi.
آية رقم 21
Basi hali zenu zisiwe namna hiyo. Kumbukeni pindi ardhi itakapotikiswa na kuvunjwavunjwa.
آية رقم 22
ﯽﯾﯿﰀﰁ
ﰂ
Na Akaja Mola wako kutoa uamuzi kwa waja Wake hali Malaika wamepiga safu.
آية رقم 23
Na ukaletwa, Siku Hiyo kubwa, moto wa Jahanamu. Hiyo ndiyo Siku kafiri atakumbuka na kutubia. Kutamfalia nini sasa kukumbuka kwake na kutubia, na yeye katika ulimwengu alikuwa ameyapuuza hayo, na wakati wake umekwisha kupita?
آية رقم 24
ﭜﭝﭞﭟ
ﭠ
Atakuwa akisema: ‘Laiti mimi nilitanguliza ulimwenguni amali zenye kunifaa katika maisha yangu ya Akhera’.
آية رقم 25
ﭡﭢﭣﭤﭥ
ﭦ
Katika Siku Hiyo ngumu yenye vituko, hakuna atakaye kuweza kuadhibu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa anayemuasi.
آية رقم 26
ﭧﭨﭩﭪ
ﭫ
Na hakuna atakaye kuweza kufunga kama kifungo Chake wala kufikia hadi yake.
آية رقم 27
ﭬﭭﭮ
ﭯ
Ewe nafsi iliyotulia kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, kumwamini Yeye na kuamini starehe ya Pepo Aliyowaandalia waumini!
آية رقم 28
ﭰﭱﭲﭳﭴ
ﭵ
Rudi kwa Mola wako hali ya kuridhika na takrima ya Mwenyezi Mungu kwako na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Ameridhika na wewe.
آية رقم 29
ﭶﭷﭸ
ﭹ
Ingia miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu walio wema
آية رقم 30
ﭺﭻ
ﭼ
na ingia kwenye Pepo yangu.
تقدم القراءة