ترجمة معاني سورة البينة باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
ﰡ
آية رقم 1
Hawakuwa wenye kukufuru miongoni mwa Mayhudi na Wanaswara na washirikina ni wenye kuacha ukafiri wao mpaka uwajilie wao ushahidi walioahidiwa katika vitabu vilivyopita.
آية رقم 2
ﮤﮥﮦﮧﮨﮩ
ﮪ
Nao ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, atakayewasomea Qur’ani iliyomo kwenye kurasa safi.
آية رقم 3
ﮫﮬﮭ
ﮮ
Ndani ya kurasa hizo mna habari za kweli na amri za uadilifu zenye kuongoza kwenye haki na kwenye njia ilionyoka.
آية رقم 4
Na hawakutofautiana wale waliopewa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, juu ya kuwa Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni Mtume wa kweli, kwa sifa zake waliokuwa wakiziona katika vtabu vyao isipokuwa baada ya kuwathibitikia kuwa yeye ndiye Nabii waliyoahidiwa katika Taurati na Injili. Walikuwa wanakubali , kwa umoja wao, kuwa unabii wake ni wa kweli. Lakini alipotumilizwa waliukanusha na wakatofautiana.
آية رقم 5
Na hawakuamrishwa katika sheria zote zilizopita isipokuwa ni wamuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake, wakikusudia kwa ibada yao kupata Radhi Zake, hali ya kuepuka upande wa ushirikina na kuelekea kwenye Imani, wasimamishe Swala na watoe Zaka. Kufanya hayo ndio Dini iliyolingana , nayo ni Uislamu.
آية رقم 6
Hakika wale waliokufuru miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara na Washirikina, mateso yao ni Moto wa Jahanamu. Watakuwa ni wenye kukaa milele humo. Wao ndio viumbe waovu kabisa.
آية رقم 7
Hakika wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakamfuata Mtume wake na wakafanya amali njema, wao ndio bora wa viumbe.
آية رقم 8
Malipo yao , mbele ya Mola wao Siku ya Kiyama, ni Pepo ya makazi na utulivu yenye upeo wa uzuri, ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito; watakaa milele humo. Mwenyezi Mungu Ameridhika nao Akakubali amali zao njema. Na wao wameridhika na Yeye kwa maandalio Aliyowafanyia ya aina mbalimbali za takrima. Malipo mazuri hayo ni ya aliyemuogopa Mweyezi Mungu na akajiepusha na maasia.
تقدم القراءة