ترجمة معاني سورة الهمزة باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

آية رقم 1
Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatukana.
آية رقم 3
Akidhani kuwa mali yake ambayo ameyakusanya yatampa dhamana ya kuishi milele duniani na kuhepa kuhesabiwa.
آية رقم 4
Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa.
آية رقم 5
Lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni upi huo Moto unaovunjavunja?
آية رقم 6
Huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa.
آية رقم 7
Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini ukafikia kwenye nyoyo.
آية رقم 8
Moto huo umefungiwa juu yao wakiwa wametiwa minyororo
تقدم القراءة