قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ
Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Hakika huyo ni mchawi mjuzi.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Watukufu wa watu wa Fir'awn walisema, «Hakika Mūsā ni mchawi, anayatawala macho ya watu kwa kuwadanganya mpaka ikawaingia kwenye fikira zao kuwa fimbo ni nyoka, na kukiona kitu kinyume na vile kilivyo, na yeye ana ujuzi mwingi wa uchawi na ana uhodari nao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس