قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ نَحۡنُ ٱلۡمُلۡقِينَ
Wakasema: Ewe Musa! Je, utatupa wewe, au tutakuwa sisi tutao tupa?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wakasema wachawi wa Fir'awn kumwambia Mūsā, kwa njia ya kujiona na kutojali. «Ewe Mūsā, chaguwa uwe ni wa mwanzo kutupa fimbo yako au tuwe sisi ni wa mwanzo kutupa.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس