قَالُوٓاْ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ
Wakasema: Sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Walisema wachawi kumwambia Fir'awn, «Tuna uhakika kwamba sisi ni wenye kurejea kwa Mwenyezi mungu na kwamba adhabu Yake ni kali zaidi kushinda adhabu yako. Tutasuburi kikwelikweli leo kwa adhabu yako, tupate kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس