وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيۡهِمُ ٱلرِّجۡزُ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَۖ لَئِن كَشَفۡتَ عَنَّا ٱلرِّجۡزَ لَنُؤۡمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرۡسِلَنَّ مَعَكَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ
Na ilipo waangukia adhabu wakasema: Ewe Musa! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa aliyo kuahidi. Ukituondolea adhabu hii hapana shaka tutakuamini, na tutawaachilia Wana wa Israili wende nawe.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na adhabu ilipomteremkia Fir'awn na watu wake, walimkimbilia Mūsā na wakasema, «Ewe Mūsā, tuombee Mola wako, kwa wahyi aliokuletea Mwenyezi Mungu kwamba adhabu huondolewa kwa kutubia. Na ukituondolea adhabu tuliyonayo, tutayaamini uliyokuja nayo, na tutayafuata uliyotuitia kwayo, na tutawaachilia, pamoja na wewe, Wana wa Isrāīl, hatutawazuia waende na wewe pale wanapotaka.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس