قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٰطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ
Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Iblisi akasema, Mwenyezi Mungu Amlaani, «Kwa sababu ya kuwa wewe umenipoteza, nitafanya bidii katika kuwapoteza binadamu wawe kando ya njia yako iliyolingana sawa na nitawazuia wao wasiuuandame Uislamu ambao wanasibiana na umbile lao ulilowaumbia.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس