وَإِذۡ قِيلَ لَهُمُ ٱسۡكُنُواْ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةَ وَكُلُواْ مِنۡهَا حَيۡثُ شِئۡتُمۡ وَقُولُواْ حِطَّةٞ وَٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا نَّغۡفِرۡ لَكُمۡ خَطِيٓـَٰٔتِكُمۡۚ سَنَزِيدُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na pale walipo ambiwa: Kaeni katika mji huu, na mle humo mpendapo, na semeni: Tufutie dhambi zetu. Na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu, tupate kukusameheni makosa yenu. Walio wema tutawazidishia.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kumbuka, ewe Mtume, uasi kwa Wana wa Isrāīl Mola wao, kutakata na sifa pungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, na Nabii wao Mūsā, amani imshukiye, na kugeuza kwao maneno waliyoamrishwa wayaseme pindi Alipowaambia Mwenyezi Mungu, «kaeni mji wa Baitul Maqdis na kuleni matunda yake, nafaka zake na mimea yake popote mtakapo na wakati wowote mtakao na semeni, ‘tuondoshee dhambi zetu,’ na ingieni mlangoni mkimnyenyekea Mwenyezi Mungu, tutawasamehe makosa yenu na hatutawaadhibu kwayo, na tutawaongezea walio wema kheri mbili: za ulimwengu na Akhera.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس