وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوۡمَهُۥ لِيُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبۡنَآءَهُمۡ وَنَسۡتَحۡيِۦ نِسَآءَهُمۡ وَإِنَّا فَوۡقَهُمۡ قَٰهِرُونَ
Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Unamuacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na wakuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawauwa wavulana wao, na tutawaacha hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Watukufu na wakubwa miongoni mwa watu wa Fir'awn walisema kumwambia Fir'awn, «Unamuacha Mūsā na watu wake, Wana wa Isrāīl, wawaharibu watu katika nchi ya Misri kwa kuwageuzia dini yao na kuwaletea ibada ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, Asiye na mshirika, na kuacha kukuabudu wewe na kuwaabudu waungu wako?» Fir'awn akasema,»Tutawaua watoto wa kiume wa Wana wa Isrāīl, na tutawaacha watoto wao wa kike waishi ili watumike; na sisi tuko juu yao kwa nguvu za ufalme na mamlaka.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس