وَمِن قَوۡمِ مُوسَىٰٓ أُمَّةٞ يَهۡدُونَ بِٱلۡحَقِّ وَبِهِۦ يَعۡدِلُونَ
Na katika kaumu ya Musa lipo kundi linao waongoa watu kwa haki na kwa haki wanafanya uadilifu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na miongoni mwa Wana wa Isrāīl wanaotokana na jamaa za Mūsā kuna kundi la watu ambao wanasimama imara juu ya haki, wanawaongoza watu kwenye hiyo haki na wanafanya usawa katika kutoa uamuzi katika mambo yao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس