ٱدۡعُواْ رَبَّكُمۡ تَضَرُّعٗا وَخُفۡيَةًۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ
Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi warukao mipaka.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Muombeni, enyi Waumini, Mola wenu, kwa kujidhalilisha Kwake, kwa siri na kwa dhahiri.Na maombi yawe kwa unyenyekevu na yawe mbali na kujionyesha.Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi wanaokiuka mipaka ya sheria Zake. Na ukiukaji mkubwa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kama vile kuwaomba wafu, masanamu na wengineo mfano wao wasiokuwa Mwenyezi Mungu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس