۞هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ وَجَعَلَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا لِيَسۡكُنَ إِلَيۡهَاۖ فَلَمَّا تَغَشَّىٰهَا حَمَلَتۡ حَمۡلًا خَفِيفٗا فَمَرَّتۡ بِهِۦۖ فَلَمَّآ أَثۡقَلَت دَّعَوَا ٱللَّهَ رَبَّهُمَا لَئِنۡ ءَاتَيۡتَنَا صَٰلِحٗا لَّنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ
Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu. Na anapo muingilia hubeba mzigo mwepesi, akitembea nao. Anapo kuwa mja mzito, wote wawili humwomba Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wao: Kama ukitupa mwana mwema tutakuwa katika wanao shukuru.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Yeye Ndiye ambaye Aliyewaumba nyinyi, enyi watu, kutokana na nafsi moja, nayo ni Ādam, amani imshukiye. Na akaumba kutokana na nafsi hiyo ya pili yake, nayo ni Ḥawwā’, ili aliwazike naye na ajitulize. Alipomuundama - makusudio ni jinsi ya mke na mume miongoni mwa kizazi cha Ādam - alibeba maji mapesi, akainuka nayo na akakaa nayo mpaka mimba ikatimia. Kilipokaribia kipindi cha kuzaa kwake na akawa mzito, walimuomba, mume na mke, Mola wao, «Tunaapa lau utatupatia mwanadamu aliye sawa, aliye mwema, hakika tutakuwa ni wenye kukushukuru kwa kutupa mtoto mwema.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس