قَالَ إِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ
Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Akasema Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, «Wewe ni miongoni mwa wale niliowaandikia kucheleweshwa kipindi chao cha kufa mpaka Mvivio wa Kwanza katika Parapanda pindi viumbe wote watakapokufa.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس